TANGAZO
Mtu
mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa baada bas
la kampuni ya Dar Lux likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana
uso kwa uso na mistubishi fuso katika eneo la njia panda ya Berega
wilaya ya Gairo barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
Kwa
mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifas mbao amesema
aliye fariki ni abiria aliye kuwa kwenye basi na chanzo cha ajali ni
mwendo kasi wa dereva wa fuso alitaka kulipita gari jingine bila
tahadhari na kusababisha ajali ya uso kwa uso.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa fuso
ambapo gari ilimshinda kutokana na utelezi katika eneo la Berega na
kusababisha ajali hiyo.
KUTOKA EDDY BLOG
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment