} });
 

TANGAZO

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (kushoto), akimtambulisha Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael kwamba ndiye atakayerithi mikoba yake katika uchaguzi mkuu ujao.Picha na Dionis Nyato.
Moshi. Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo, juzi alifanya tukio la aina yake pale alipomtangaza Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael kuwa ndiye atakayerithi mikoba yake.
Tangazo hilo sasa linavunja minong’ono iliyokuwa imezagaa kwamba Ndesamburo hatagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, baada ya kuliwakilisha jimbo hilo kwa miaka 15 kuanzia 2000.
Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Kilimanjaro alimtangaza Michael katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Manyema kuwa ndiye anatamani awe mrithi wake.
“Niwatafutieni mbunge nisiwatafutie? Niwatafutieni mrithi wangu niache? Nimtaje nisimtaje?”, hayo ndiyo maneno aliyoyatumia Ndesamburo kuwauliza wananchi kama amtaje mrithi wake au la.
“Mtaniunga mkono kwamba nitakayemtaja ndiye mtakayemsaidia? Jaffar njoo hapa bwana (akimwita Meya). Sasa nawaambia wakati ukifika ndio huyu nitakayemfanyia kampeni,” alisema Ndesamburo.
Huku akiwa amemnyanyua mkono, Ndesamburo alisema muda ukifika atamleta Michael mbele ya wananchi ili wamfanyie kampeni. Kauli hiyo ilifanya umati uliohudhuria mkutano huo kulipuka kwa furaha.
“Nimefanya hivi kwa ajili ya kuondoa majungu, kwa ajili ya kuondoa makundi na kwa ajili ya kujenga umoja wa chama chetu,” alisema huku akimsifia kuwa ni mtu msafi na anayewajibika kwa wananchi.
Hata hivyo, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema alipoulizwa jana kuhusu uamuzi huo wa Ndesamburo alisema haikuwa sahihi kumtangaza mrithi akisema ni kinyume cha Katiba yao.
“Ninakubali maoni yake binafsi kama binadamu, lakini kama mwenyekiti wa mkoa haikuwa sahihi kwa sababu hiyo ni kinyume cha Katiba. Akifanya hivyo anaminya demokrasia ndani ya chama,” alisema.
Mkazi wa Pasua Relini, Charles Mboya alipoulizwa na gazeti hili amechukuliaje uamuzi huo wa Ndesamburo alisema Meya huyo anakubalika na ndio maana hata Rais Jakaya Kikwete alimfagilia.
“Kama Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa taifa wa CCM alimfagilia Meya huoni hilo ni jembe? Kwa kweli mimi namkubali kwa sababu ni mtu mwenye msimamo thabiti,” alisema Mboya.
Februari 10, wakati Rais Kikwete akizindua jengo la kitega uchumi la Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF), alimsifu Meya kwa kutekeleza vizuri ilani ya ‘CCM’ na kuahidi kuiongezea pesa Halmashauri.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top