TANGAZO
22.04.2015 00:00
Maafisa tisa wa Kenya wamesimamisha kazi na huenda wakakabiliwa na mashtaka ya uzembe uliosababisha uhalifu wa mauaji yaliyofanyika mapema mwezi huu katika chuo kikuu cha Garissa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la ufaransa, serikali ya Kenya jana imesema wafanyakazi wawili wa serikali na maafisa saba waandamizi wa polisi huko Garissa inaonekana walishindwa kujiweka sawa kabla ya shambulizi licha ya maonyo ya mapema ya kipelelezi.
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, Joseph Nkaissery amesema ametoa onyo kwa maafisa wote waliopewa jukumu la ulinzi nchini humo watawajibishwa kwa vitendo vyovyote ambavyo vitahatarisha maisha na mali za wakenya.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment