} });
 

TANGAZO
Mh.James Lembeli
Mbunge wa Jimbo la Kahama mh.James Lembeli,imethtibika kuwa ni mpambanaji kwa ajili ya kupigia haki na masilahi ya wananchi (jembe la wananchi) asiejali chama wala itikadi ya kidini.
Yamethibitika hayo wakati akihutubia wananchi wa kata ya Majengo Wilayani Kahama.Waziwazi kweupe Mh.Lembeli amewashutum viongozi wa chama chake kata ya Majengo kwa kutohudhuria katika mkutano huo ulioandaliwa na Mkombozi saccos.Mh.Lemmbeli amesema kinachomsikitisha ni jinsi ambavyo kiongozi akisema ukweli anaambiwa ni mpinzani.
Kawaomba wananchi washirikiana kwa pamoja katika kuiletea maendeleo Wilaya ya Kahama nakuomba wasifanye kosa katika uchaguzi ujao na wachague mtu mchapa kazi atakayefanya kazi ya wananchi na sio kufanya kazi yakubwa fulani walioko juu.
Mh.Lembeli alisema "kwanza natambua kata ya Majengo kimaendeleo iko mkiani hakuna maendeleo hapa,lakini la pili sioni kiongozi wa kata ukiacha mtendaji na hata wala wa chama changu,najua
diwani wake anatoka chama cha CHADEMA na yeye hajaonekana" Mh.Lembeli alisikitishwa na kitendo hicho
Lembeli Jembe

Katika kikundi hicho cha Mkombozi Saccos Mheshimiwa aliahidi kuwapa Tshs.3000000 kwa ajili yakuhakikisha kikundi hicho kinasonga mbele na kusisitiza hizo pesa zitumike kwa ajili yakununua vifaa lengwa.Hata hivyo mtendaji wakata ya Majengo aliomba msaada wa madawati pamoja na choo kwaajili ya shule ya msingi Majengo ambayo inajumla ya wanafunzi 1400 na ikiwa na vyumba vinane vya madarasa na matundu sita ya choo ambapo mpaka sasa kuna mahitaji ya matundu 12 kuongezwa angalau kupunguza tatizo la choo kwani iko hatarini kufungwa kutokana na tatizo hilo na uwezo walionao ni kujenga tundu 6 tu,ambapo Mh.Lembeli alisema mpaka wakae nae ndo ajue namna ambavyo ataweza kusaidia.
Wananchi walitokea kuvutiwa sana nahotuba la mh.Lembeli haswa alipotoa fursa ya wananchi kuuliza maswali ya papo hapo na wananchi wengi wameahidi kuwa nae katika kupigania haki.....

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top