} });
 

TANGAZO
Mwanza. Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu amedai kuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na wabunge wenzake wa upinzani mkoani hapa kwa miaka minne ya uwepo wao bungeni, wameshindwa kutekeleza ahadi zao.
Pia, amedai kuwa ahadi zilizotolewa na wabunge hao mwaka 2010, zilikuwa sawa na nyimbo za taarabu, kwa kuwa hazikutekelezwa.
Pia akisema wabunge hao wamegeuza mifuko ya Jimbo kuwa mali zao.
Katibu huyo alisema CCM inajipanga kuyakomboa majimbo hayo ya Nyamagana, Ilemela na Ukerewe ambayo yanayoongozwa na wapinzani ili kuwaletea wananchi maendeleo endelevu..
Hata hivyo Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje alisema anatambua CCM, Mwanza hawawezi kuwasema wapinzani vizuri.
“Katika majimbo yote hapa nchini Jimbo la Nyamagana ni namba moja kwa matumizi mazuri ya fedha za mfuko wa Jimbo wananchi wanajua, hata kama CCM hawajui hilo.Mimi natambua kwamba Katibu wa CCM na wenzake hawezi kunisema vizuri kwa sababu wanajua nguvu yangu inawanyima usingizi,” alisema Wenje.
Alichosema Katibu CCM
Katibu huyo wa CCM alisema “Ndugu zangu nimekuja kuwaambia kwamba mwaka 2010 mlikosea kufanya uamuzi wa kuwaweka wabunge wa upinzani Mwanza, kwani hawajafanya kitu yote waliyoyahidi zilikuwa taarabu,” alisema Mtaturu kuongeza:
“Siasa siyo ushabiki wa mpira wanasiasa wanatakiwa kutumia majukwaa ya kisiasa vizuri.”
Katika hali ya kushangaza wakati Katibu huyo akihutubia kikundi cha baadhi ya vijana waliyokuwa wamekaa pembeni waliibuka na kuzomea, huku wakipiga vuvuzela baada ya Katibu huyo kumfananisha Wenje na Wanja ambao ni moja ya kipodozi cha wanawake.
“Huyu Wenje ni sawa na Wanja au sio…jamani maana Wanja kazi yake ni kujipodoa tu na hakuna kazi nyingine,” alisema..huku kikundi kicho kikimzomea.
Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alisema kuwa kipindi hiki cha ukelekea kwenye uchaguzi mkuu wanamwanza wasikubali kudanganywa tena, kwani wameshuhudia wenyewe viongozi waliyowachagua kitu gani wamefanya.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top