TANGAZO
Watu 19 wamekufa na wengine wanne wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Hiace kuanguka katik eneo linaloitwa Uwanja wa Ndege , Kiwira Mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Bwana AHMED MSANGI amesema watu 18 wamekufa papo hapo na mmoja amefariki dunia akiwa njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Misheni ya Igogwe kwa matibabu.
Kamanda MSANGI amesema kulikuwemo abiria 21 kwenye Hiace hiyo na miongoni mwa waliokufa ni dereva wa gari hiyo na ameongeza majeruhi aliozungumza nao wamemweleza walimtaka dereva apunguze mwendo,lakini hakupunguza mwendo.
Amesema kutokana na mgomo wa mabasi makubwa Mkoani Mbeya dereva huyo alitumia nafasi hiyo kubeba abiria hao ambao walikuwa wanakwenda mnadani.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo chake ni mwendo kasi, huku akiwata madereva kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment