} });
 

TANGAZO
Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kimesema ni aibu kubwa kwa taifa kama Tanzania linalo sifika katika demokraisa amani na uwazi kupitisha mswada wa sheria ya kuvibana vyombo binafsi  vya habari na hii inaonesha namna serikali ya CCM inavyoogopa kukosolewa katika maovu wanayo yafanya ili waendelee kuwanyonya wananchi na kuwanyima taarifa wasipate ufahamu.
Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalimu ametoa kauli hiyo katika mikutano ya hadhara ya chama hicho iliyofanyika katika miji ya Basutu na Endesaki wilayani Hanang na kusema ni kitendo cha aibu wakati nchi nyingine duniani zinafanya jitihada za kuboresha uwazi katika sekta ya habari Tanzania inayo jinasibu kwa demokrasia inavibana vyombo vya habari.
 
Aidha Salum Mwalim amesema serikali inachotakiwa kufanya ni kuboresha vyombo vya habari vya  serikali viweze kufanya taarifa zitakazo kubalika na jamii ili viingie katika ushindani tofauti na ilivyo sasa lasivyo watakuwa wanamtafuta mchawi mpaka mwisho wa dunia.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema kanda ya kaskazini mchungaji Israel Natse amesema huu ulikuwa ni wakati waserikali kuangalia makosa waliyo fanya kwa wananchi lakini ajabu wananchi wanabanwa huku wahujumu kama wa akaunti ya Eskrow wanasafishwa kwa nguvu kubwa.                                                                             
 

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top