} });
 

TANGAZO
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeanza kutoa elimu kwa wadau wa mawasiliano nchini ili kujiandaa kwa biashara ya wazi ya masafa ya mawasiliano ifikapo Oktoba, mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema mamlaka hiyo itaanza kuuza masafa hayo kwa wadau wake ambao ni kampuni za simu za mkononi, redio na televisheni.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukabiliana na changamoto ya mahitaji ya masafa ya mawasiliano, ambayo kwa sasa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji.
Profesa Nkoma alisema wadau hao watakuwa na fursa ya kulipia masafa hayo kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa na TCRA vinavyochagizwa na mabadiliko ya tenkolojia mpya ya mawasiliano.
“Faida za kufanya mnada kwa uwazi na haki ni kutaka kuepuka malalamiko ya wadau, kila mdau anahitaji kupata masafa lakini yapo kidogo, masafa hayo yanaanzia 694MH mpaka 862MH. Kila mmoja atapata kwa kuzingatia vigezo, lakini kabla ya kufikia hatua ya mnada huo, leo (jana) tutatoa elimu juu ya ugawaji na vigezo ili wavifahamu pamoja na mambo mengine,” alisema Profesa Nkoma.
Kwa upande wake, Mhandisi Masafa kutoka mamlaka hiyo, Victor Kweka alisema mbali na faida hizo, nyingine ni kupunguza matumizi ya kuwa na minara mingi ya kampuni za simu katika eneo lenye umbali mfupi.
“Yote haya ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia kukua zaidi kutoka analojia kwenda dijitali,” alisema Kweka.
“Masafa hayo yatasaidia kuongeza kasi ya kufika mbali zaidi na kwa urahisi ukilinganisha na ilivyo sasa, kampuni zinatumia minara mingi na wakati mwingine wananchi huilalamikia.”

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top