TANGAZO

BARAZA Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), limemvua uanachama mjumbe wake kutoka Mkoa wa Shinyanga, Chifu Lutayosa Yemba.
Chifu
Yemba ambaye pia alikuwa ni mpinzani wa Profesa Ibrahim Lipumba katika
kuwania uenyekiti wa CUF kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana,
alivuliwa uanachama kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za chama pamoja na
kutumia vibaya jina la mwenyekiti wa chama hicho.
Chanzo
cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho cha Baraza Kuu kilichoanza
vikao vyake jana jijini Dar es Salaam, kimesema kuwa tuhuma za mjumbe
huyo zilifikishwa mbele ya kikao hicho na kufikiwa uamuzi huo.
“Kikao
cha Baraza Kuu bado kinaendelea hapa na ajenda kubwa ilikuwa ni tuhuma
dhidi ya Chifu Yemba ambaye anadaiwa kutumia jina la Mwenyekiti wa chama
kuanzisha Saccos na hata kusababisha chama kudaiwa shilingi milioni 12.
“Lakini
pia amekuwa akitumia jina la Mwenyekiti wa chama, Profesa Lipumba
katika mradi wake huo binafsi ambao anauendesha na hata kusababisha
chama kuingia katika mgogoro hasa katika Mkoa wa Shinyanga,” kilisema chanzo hicho.
Chifu
Yemba alipambana na Profesa Lipumba katika uchaguzi wa kuwania nafasi
ya uenyekiti ambapo alipata kura 30 huku Lipumba akishinda kwa kura 659
na kufanikiwa kukiongoza tena chama hicho.
Chanzo
hicho kilisema baada ya kufikiwa kwa uamuzi wa kuvuliwa uanachama kwa
Mjumbe huyo wa Baraza Kuu, alitolewa nje ya ukumbi kwa ulinzi maalumu
hadi nje ya geti na kuondoka.
Yemba
kwa muda amekuwa haelewani na hata kushambuliana katika mitandao ya
kijamii na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Abdul Kambaya ambaye
hivi karibuni alishindwa kura za maoni za kuwania ubunge wa Jimbo la
Kinondoni.
Kutokana
na kushindwa huko kwa Kambaya, kuliibua hisia mbalimbali miongoni mwa
wana CUF hali iliyosababisha baadhi ya kikundi cha watu kuandamana na
kwenda Makao Makuu ya CUF kufikisha malalamiko yao kuhusu mwenendo wa
uchaguzi Kinondoni.
Alipotafutwa
Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya,
alithibitisha kuvuliwa uanachama kwa Chifu Yemba na kikao cha Baraza Kuu
la Uongozi la CUF.
“Ni
kweli tumemfukuza uanachama mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Shinyanga kwa
tuhuma mbalimbali, tutatoa taarifa rasmi kesho kutwa (kesho) kwa sababu
kesho (leo) tunaenda mahakamani,” alisema Kambaya.
Pamoja na kufikiwa kwa uamuzi huo, mwandishi alimtafuta Chifu Yemba ambaye alithibitisha kufukuzwa kwake uanachama ndani ya CUF.
“Tatizo
wana shaka na mimi sana, tuhuma zao zote hazina mashiko, katika
mashtaka nilikubali moja tu la kutumia nembo ya chama, ni kweli na
nikabadilisha sijaelewa jina la Profesa Lipumba nimelitumia vipi,
wamepanga kuathiri taasisi na wataniathiri kwa kweli.
“Mimi
sina tatizo na CUF, naipenda katika moyo wangu lakini wao hawanipendi
na wamefanya maamuzi kikatiba, ila hizi ni hujuma za Kambaya (Abdul) na
Sakaya (Magdalena) ambao ndio walipanga kuhakikisha natoka CUF na
wamefanikiwa.
“…
unajua mimi ni mwanasiasa, natafakari kwa kina hatua za kuchukua baada
ya kutokea hili. Na kwa sasa najipanga kuendelea na maisha mengine ya
kisiasa nje ya CUF,” alisema Chief Yemba.
CHANZO EDDY BLOG
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment