TANGAZO
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) lipo mbioni kumtaja kocha atakayerithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa Stars, Mdachi Mart Nooij ili kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Uganda ya kufuzu kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Rwanda.
Tetesi zilizopo ni kwamba makocha wazawa, Charles Boniface Mkwasa na Suleiman Matola huenda wakapewa jukumu hilo zito kwa muda na kuiandaa timu dhidi ya Uganda.
Mkwasa amekiri kuhusishwa kwake na Stars na amenukuliwa akisema yupo tayari endapo atapewa barua rasmi kuiongoza timu hiyo mpaka atakapopatikana kocha mwingine.
Mabao mawili ya mshambuliaji Erisa Sekisambu na lingine la Farouk Miya yaliiwezesha Uganda kushinda 3-0 Jumamosi visiwani Zanzibar na yalihitimisha kazi ya Mholanzi huyo nchiniTanzania baada ya kukatishwa mkataba wake na TFF kufuatia rekodi ya kufungwa mfululizo zaidi ya mechi nne mfululizo hivi karibuni.
Kwa ujumla, Nooij ameiongoza Stars katka mechi 18 tangu kati ya hizo ameshinda tatu tu, sare sita na kufungwa tisa- akifunga mabao 17 na kufungwa 28.Mechi ya marudiano baina ya Stars na Cranes itachezwa wiki mbili zijazo jijini Kampala, nchini Uganda.
Tanzania sasa inatakiwa kwenda kushinda mabao 4-0 ugenini wiki mbili zijazo ili kusonga mbele Raundi ya Kwanza. .
Mkwasa kwa sasa ni kocha msaidizi wa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wakati Matola, aliyewahi kucheza soka la kulipwa nchini Afrika ya Kusini, ni kocha msaidizi anayeiongoza klabu ya Simba.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment