TANGAZO
UKOSEFU wa nyumba za watumishi katika Sekta ya Afya hasa maeneo yenye miundombinu duni ya usafiri kunakofanya watumishi kushindwa kukaa katika maeneo hayo, kumetajwa kuwa ni moja ya mambo yanayochangia kuongeza vifo vya wajawazito na watoto.
Kutokana na hali hiyo, Serikali mkoani Kigoma imeanza mkakati wa ujenzi wa nyumba 70 za watumishi wa afya, lengo likiwa kuhakikisha wataalamu katika Sekta ya Afya wanapatikana maeneo yote ya utoaji huduma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya alisema hayo wakati akipokea nyumba moja yenye uwezo wa kuishi familia mbili kwa ajili ya watumishi wa afya kwenye Kituo cha Afya Nguruka Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma na kusema kuwa ujenzi huo kwa kiasi kikubwa utatumia nguvu za wananchi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Lung, Dk Nguke Mwakatundu alisema kuwa pamoja na ujenzi wa nyumba hiyo iliyogharimu Sh milioni 156 pia wamejenga nyumba nyingine katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
Dk Mwakatundu alisema kuwa uboreshaji miundombinu kumesaidia kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment