TANGAZO
Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu amemshtaki aliyewahi kuwa
mchumba wake Faiza Ally na aliyezaa naye mtoto kwa madai kuwa mwanamke
huyo hana maadili na anahofia atamharibu mtoto wao. Sugu anataka
kumchukua mtoto huyo na aishi naye (child custody).
Faiza
ameiambia Bongo5 kuwa baada ya siku chache zilizopita kupandishwa
kizimbani na kujibu shtaka hilo, alisema yeye hawezi kukubali kumuachia
Sugu mtoto huyo kwa kuwa yupo chini ya umri.
“Kweli
Sugu amenipeleka mahakamani kumtaka mtoto,” amesema Faiza. “Mimi naona
ni mtu anayekwepa majukumu kwa sababu chanzo cha yote nilikuwa namkata
atulipie kodi ya nyumba, kwa sababu toka tuachane hajawahi kulipa kodi
ya nyumba na siyo baba ambae anajali majukumu ya nyumbani kama
inavyotakiwa.”
“Kwahiyo
nilivyoanza kumshauri kuhusu hilo akaniambia yeye anaweza kumchukua
mtoto wake na mali zake anaweza kumlea mtoto wake. Sasa nilivyobishana
naye kuhusu hilo wiki moja baadaye ndo likaja ili suala la KTMA ndio
akalichukulia kama sababu ya kuweza kupeleka suala mahakamani kwa kudai
sina maadili, kwahiyo nitammharibu mtoto. Kwahiyo kesho Jumanne ndio
hakimu anatoa hukumu juu ya hili.
Lakini
mtoto bado ni mdogo ana miaka miwili na kama miezi tisa bado mdogo
anahitaji malezi yangu, pia hili suala nitalipeka ustawi wa jamii ili
waangalie haki ya malezi ya mama kwa mtoto.”
Chanzo: Bongo5.com
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment