} });
 

TANGAZO


  Timbwili la aina yake lilizuka mwishoni mwa wiki iliyopita baada njiwa aliyekuwa amefungwa hirizi na barua iliyokuwa imeandikwa kwa Lugha ya Kiarabu kuzunguka katika baa zipatazo 26 zilizopo Banana, wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka eneo hilo, njiwa huyo alizunguka katika kila baa iliyopo eneo hilo na mwisho alitua jirani ya baa moja.
 
Kabla ya kutua katika paa za baa hizo, baadhi ya watu waliokuwa wakipata kinywaji walisema njiwa huyo alionekana kwa muda mrefu akiwa  anaruka na vitu vyeupe kwenye mbawa zake.
 
Mmoja wa wateja katika baa hiyo alisema licha ya kumuona ndege huyo hawakujali  na  badala  yake  walimkamata  na kumwondolea hirizi na karatasi.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top