TANGAZO
TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kimataifa wa vitambulisho vya taifa vya kielektroniki barani Afrika (ID4Africa).
Mkutano huo wa siku tatu utaanza leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe anatarajiwa kufungua mkutano huo.
Akizungumza kuhusu mkutano huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mfumo wa Kompyuta wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Joseph Makani alisema mkutano huo ni wa kwanza kufanyika barani Afrika.
“Tanzania tumepata heshima ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufanya mkutano huu wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki baada ya mabara ya Asia na Ulaya kuendesha mikutano hiyo kila wakati na Afrika kwenda kushiriki huko,” alisema Makani.
Mkutano huo utawaleta pamoja wadau mbalimbali, zikiwepo mamlaka za vitambulisho, serikali, taasisi za fedha na taasisi za maendeleo za kimataifa.
Makani alisema katika mkutano huo, masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na changamoto mbalimbali, zitokanazo na uendeshaji wa utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa nchi za Afrika.
“Zipo changamoto za aina mbalimbali ambazo kila nchi inakabiliana nazo katika hili, hivyo itakuwa ni fursa ya nchi washiriki kujadili kwa pamoja namna ya kukabiliana na changamoto hizo,” alisema Makani.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment