} });
 

TANGAZO


Idadi ya wahamiaji imeongezeka maradufu
Mashirika mawili ya kimataifa yanasema idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya kupitia njia zisizo halali za kupitia pwani ya Mediterranea kufikia sasa imepita laki moja mwaka huu .
Mashirika hayo mawili UNHRC na lile linalohusika na wahamiaji IOM yametoa takwimu hizo zinazofanana kwa idadi ya wahamiaji wanaofikia kwanza Uitaliano na kisha Ugiriki.
IOM inasema takwimu hizo zaonesha ongezeko maradufu ikilinganisha na idadi ya wahamiaji mwaka uliopita wa 2014.
Wahamiaji wanaofikia Italia wanatokea Eritrea huku wale wanaofikia Ugiriki wanatokea Syria na Afghanistan
Aidha mashirika hayo yameonya kuwa idadi kubwa zaidi ya wahamiaji wanatarajiwa katika miezi ijayo.
Wengi wa wahamiaji wanaofikia kwanza Italia wanatokea Eritrea huku wale wanaofikia kwanza Ugiriki wanatokea Syria na Afghanistan.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top