TANGAZO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ameshauri vijana kuunda vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo na kufanya shughuli za maendeleo.
Aidha aliwataka vijana kuacha kukaa vijiweni kupiga porojo na kujadili siasa, badala yake wajitume kwa kufanya kazi waondokane na umasikini.
Alisema hakuna chama cha siasa kitakachoweza kuwalipa mishahara bila kufanya kazi na pia hakuna njia ya mkato bila ya kufanya kazi.
Kinana alitoa mwito huo juzi katika maeneo mbalimbali wilayani Nyang’hwale wakati akizindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wanawake.
Alisema vijana wanapaswa kuiga mfano wa akinamama, ambao wamekuwa wakipambana na umasikini kwa kujiunga na vikundi vidogo vidogo vinavyowawezesha kupata mikopo.
“Hakuna chama cha siasa kinachoweza kukupa ajira kijana wala kukulipa mshahara zaidi ya wewe kunyanyuka kijiweni na kufanya kazi, acheni kudanganywa na vyama vya siasa vya upinzani kuwa watawasaidia hakuna kitu kama hicho,” alisema Kinana.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment