} });
 

TANGAZO
Andrew Change(kushoto) akipangua hoja za mwanasheria wa serikali aliye mbele ya mwenyekiti wa tume ya maadili.

Mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma, Jaji mstaafu , Hamis Msumi(katikati) pembeni yake ni viongozi wengine wa baraza hilo.
Baadhi ya viongozi na wanahabari wakifuatilia kikao hicho.
Chenge akisoma taarifa zake.
Chenge akijiandaa kuondoka mara baada ya kuahirishwa kikao.

..akisalimiana na mmoja wa viongozi wa baraza la maadili baada ya kuahirishwa.
Chenge akitoka lango kuu la Ukumbi wa Karimjee.

TUME ya Maadili chini ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar imezidi kumhoji, Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi anayemaliza muda wake anayetuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow anazodaiwa kupata kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineerung, James Rugemalira.

Awali Mwanasheria huyo alifikishwa mbele ya baraza hilo akidaiwa kukiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kupata mgawo wa fedha kutoka kwenye akaunti hiyo ambazo zinakadiriwa kuwa ni sh. bilioni 1.6.

Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji Hamis Msumi, Chenge alikanusha kuwa hahusiki na tuhuma za fedha za Escrow na wala hajawahi kuwa na mgongano wa maslahi kati ya IPTL na VIP.

Chenge alisema kuwa aliingia mkataba na Kampuni ya VIP katika kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya kampuni binafsi zilizowekeza IPL na kwamba hakuiingia mkataba wa makubaliano na kampuni hiyo ambayo iliingia mkataba na serikali.

VIA: www.globalpublishers.info

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top