TANGAZO
Shirikisho la soka nchini Limeshauriwa kuwa na mipango endelevu na mahususi kwaajili ya kuliinua soka la kitanzania na kulifanya liwe na mvuto zaidi na kufanya timu ya Taifa kuleta matokeo mazuri ya kisoka katika anga la kimataifa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu ya soka ya Yanga Jerry Muro baada ya kuanza kwa michuano ya Chalenji nchini Ethipia huku wachezaji kadha wakiwakilisha wanaokipiga katika ligi kuu soka Tanzania bara wakiwakilisha nchi zao.
Muro amesema kitika Taasisi yoyote ni muhimu kuwa na mipango na kuleta matokeo mazuri ya nchini husika lakini kwa nchi ya Tanzania hilo halipo kutokana na TFF kuendesha soka bila kuwa na mipango mahususi ya kulikomboa soka.
Muro amesema Ligi imesimama hivi sasa kitu ambacho hata klabu yao imethirika kwa wachezaji wake kuchukuliwa kushiriki michuano hii lakini TFF walikuwa na uweza wa kupanga kalenda vizuri ili kutofautisha michuano hii na ligi kuu.
"lazima kama taasisi iwe na mipango muhimu ili kuweza kusonga mbele kisoka tumeona timu yetu imecheza na Algeri lakini tumeshindwa kusonga mbele kutoka na kutokuwa na mipango endelevu ambayo kama TFF wangeweza kuiweka leo hii tungesonga mbele",alisema Muro.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment