TANGAZO
Wasanii hao wakihojiwa.
DAR ES SALAAM: Kama hukuipata kwa kina habari ya wasanii 22 wa kucheza
ngoma za asili kutoka Sumbawanga na Makambako, Risasi Jumamosi lina full
stori ya wasanii hao ambao wamejikuta katika wakati mgumu baada ya
kutapeliwa na kuletwa jijini Dar kwa kile walichoambiwa kwamba
wanasafirishwa kuelekea nchini Misri kufanya shoo.
Chanzo
makini kilieleza kwamba, wasanii hao walisafirishwa hadi na Dar na
kutelekezwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Ponde iliyopo maeneo
ya Kigogo jijini Dar huku wakiwa na hali mbaya kwani walikuwa
wakibangaiza fedha ya kula kwa kukata mauno kwenye baa mbalimbali huku
wakisubiri mwenyeji wao awafanyie maandalizi ya kusafiri.
Baada
ya kupenyezewa habari hizo, paparazi wetu alifika katika nyumba hiyo ya
wageni ambapo watu hao walieleza kwamba waliletwa na mwenyeji wao
waliyemtaja kwa jina la Paulo Joseph Sinkala ambaye aliwaambia
anawapeleka Misri kwa ajili ya kucheza ngoma za asili.
Watu
hao ambao wanne wametokea Sumbawanga huku 18 wakitokea Makambako,
walisema Paulo alikusanya vitambulisho vyao wote na kusema kwamba
anaenda kuwatafutia hati za kusafiria ambapo kuanzia walipofika jijini
Dar Februari 12, mwaka huu hawaoni chochote kinachoendelea.
“Yaani hapa tumewekwa kwenye vyumba vitatu watu 22, tunalala kwa shida
hata kula ni kwa shida ambapo imebidi tuwe tunafanya shoo kwenye baa
mbalimbali walau tupate fedha kwa ajili ya kununua chakula,” walisema
watu hao.
Barua walioiandika kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuomba msaada
Paulo alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema kwamba yeye ni
mwenyekiti wa kikundi hicho na alikuwa anafanya mpango wa kuwasafirisha
wasanii wake hao kwenda kufanya shoo nchini Misri pia alionyesha barua
aliyoandika kwa niaba ya wenzake kwa ajili ya kumfikia Rais John
Magufuli.
Hata
hivyo, ilielezwa kuwa Paulo aliwachangisha wenzake hao kati ya sh
80,000 na 150, 000 kwa kuwarubuni kuwa kupitia kikundi chake cha
Wanyamwanga Simba Culture Group atawasafirisha kwenda kwenye tamasha la
sanaa kwa ufadhili wa rais Magufuli na mke wa rais mstaafu, Jakaya
Kikwete, Salma kitu ambacho hakikuwa na ukweli.
Paulo alishikiliwa na kituo cha polisi cha Magomeni jijini Dar kwa ajili
ya kujieleza zaidi huku watu hao wakiwa wamebaki kwenye nyumba hiyo ya
kulala wageni wakiwa hawana la kufanya.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment