} });
 

TANGAZO

*Mauaji polisi 8 Kibiti yalaaniwa, Askofu ataka waliofanya unyama huo wasakwe popote walipo *Upendo, mshikamano wahimizwa kwa Watanzania HOFU iliyoanza kujijenga katika jamii kutokana na kuwapo kwa vitendo vya utekaji watu na pia kuibuka kwa vitendo vya mauaji yakiwamo ya polisi wanane wilayani Kibiti Alhamisi iliyopita

HOFU iliyoanza kujijenga katika jamii kutokana na kuwapo kwa vitendo vya utekaji watu na pia kuibuka kwa vitendo vya mauaji yakiwamo ya polisi wanane wilayani Kibiti Alhamisi iliyopitani miongoni mwa mambo yaliyotikisa katika mahubiri baada ya ibada ya Sikukuu ya Pasaka katika makanisa mbalimbali nchini, jana. Aidha, licha ya kulaani mauaji ya polisi wasio na hatia wilayani Kibiti, Pwani na kutaka waliohusika na unyama huo kusakwa popote walipo ili wafikishwe kwenye mkono wa sheria, maaskofu na viongozi wengine walitumia mahubiri hayo ya Pasaka kuwahimiza Watanzania wazidishe upendo na mshikamano kwa nia ya kumridhisha Mungu kwa matendo hayo mema. Hivi karibuni kumetokea matukio kadhaa ya utekaji yaliyozua gumzo kubwa kuhusiana na hofu ya kutetereka kwa hali ya usalama nchini, yakiwamo ya Ben Sanaane ambaye ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyetoweka kwa zaidi ya miezi minne sasa. Mwingine aliyetekwa na watu wasiojulikana kabla ya kupatikana siku tatu baadaye ni nyota wa bongofleva, Roma Mkatoliki. Aidha, matukio ya ujambazi na mauaji dhidi ya watu wasio na hatia yaliongeza hofu nyingine Alhamisi iliyopita baada ya askari Polisi wanane waliokuwa kazini kushambuliwa kwa risasi wakiwa kwenye gari na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika eneo la Mkengeni, Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Katika tukio hilo, askari mwingine alijeruhiwa na kisha wauaji kutwaa bunduki walizokuwa nazo askari na kutokomea nazo kusikojulikana. Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac Amani; Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (Tec), Padri Raymond Saba; Askofu wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Michael Hafidh; Padri Fabian Muhoja wa parokia ya Bujora, Mwanza na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa wale waliotoa mahubiri yaliyozungumzia hali ya amani na umuhimu wa jamii kuzidisha upendo. Wengine waliotoa mahubiri ya kuhimiza upendo ni pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu; Askofu wa Kanisa la Morovian (MRCT), Emmaus Mwamakula; Mkuu wa Dinari ya Pwani Jimbo la Tanga, Moses Shemweta; Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), Dk. Dickson Chilongani.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top