TANGAZO
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akikagua Maabara ya Shule ya Sekondari Chona wilayani Kahama.
Wahandisi wa halmashauri za wilaya ya kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kukamilisha ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari walizopangiwa kabla ya juni 30,2015.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa maabara katika halmashauri ya Ushetu, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Kikwete la kujenga maabara katika shule za sekondari.
Jengo la Maabara ya Shule ya Sekondari Chona wilayani Kahama
Katika Ziara hiyo Rufunga amekagua majengo ya maabara kwenye shule 3 za sekondari katika halmashauri ya Ushetu ambazo ni Chona,Ulewe na Chambo ambapo ujenzi wake umeanza kuakamilika.
Katika halmashauri ya Ushetu amebaini Kasoro mbali mbali katika majengo ya maabara hizo na kuwataka wahandisi kwa kushirikiana na madiwani kuhakikisha wanayapatia ufumbuzi wa haraka.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiteta jambo na mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya
Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamedi Kahunge, amesema kukamilika kwa ujenzi wa maabara hizo, kutaongeza ufaulu katika masomo ya sayansi na kulifanya Taifa kuwa na idadi yakutosha ya wataalam wa sekta ya afya.
Meza za Maabara katika shule ya sekondari Chambo
Ziara ya mkuu wa mkoa imeenda sambamba na Uzinduzi wa Zahanati ya Kata ya Ulewe, ambapo ameifungua kwaajili ya kutoa huduma za afya kwa wakazi wa kata hiyo ambao hapo awali walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akifungua zahanati ya kata ya Ulewe.
Na Salvatory Kelvin wa Dunia Kiganjani Blog - Kahama
Na Salvatory Kelvin wa Dunia Kiganjani Blog - Kahama
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment