TANGAZO
Muonekano wa ghala hilo lilivyoathiriwa na mto huo.
Baadhi ya bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, katika ghala la kuhifadhia bidhaa za kampuni ya Kahama oil mills wilayani kahama.
Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake meneja mkuu wa kampuni hiyo William Matonange, amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni kuripuka kwa baadhi ya bidhaaa zenye asili ya kuripuka zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala hilo.
Aidha meneja huyo amesema kuwa bidhaa zilizoteketea zilikuwa na thamani ya zaidi ya shilling billion 3 huku jengo likiwa lenye thamani zaidi ya shilling billioni 1.
Akifafanua zaidi amesema moto huo unasadikiwa ulianza usiku wa manane ambapo uligundulika majira ya saa tisa usiku ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha zimamoto ambao walifika na kuanza kuuzima ambao ulidumu kwa masaa sita.
Hata hivyo Matonange amelipongeza jeshi la polisi mkoani shinyanga kwa juhuzi za kuimalisha ulinzi katika zoezi la kuzima moto kutokana na wananchi walikuwa na lengo la kuvamnia kiwanda hicho kwa ajili ya kwenda kupora mali wakati jeshi la zimamoto likiendelea na zoezi la kuuzima moto huo.
Kwaupande wake kamanda wajeshi la polisi mkoani shinyanga Justus Kamugisha amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa uchunguzi unaendelea hivyo taarifa zaidi zitatolewa baada ya wataalam kutoka kitengo cha bima kufanya uchunguzi wao.
Na Emmanuel Mlelekwa wa Dunia Kiganjani blog - Kahama
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment