} });
 

TANGAZO

NA CYNTHIA MWILOLEZI

Waziri wa Nishati, Madini, George Simbachawene.
Serikali imekiagiza kituo cha uongezaji thamani madini ya vito cha mkoani hapa, kutoa mafunzo kwa vijana wa kike darasa la saba na kidato cha nne bila masharti ili wapate ujuzi wa ukataji na ungarishaji madini  hayo.
 
Agizo hilo lilitolewa  jana Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, wakati akifungua  kituo hicho kilichoanza kutoa mafunzo Novemba mwaka jana.
 
Simbachawene alisema anaamini kundi kubwa la vijana wa madarasa hayo wakipatiwa kipaumbele kupewa mafunzo hayo, watajiajiri na taifa kupata mapato kwa kuyaongezea madini hayo thamani.
 
Alisema  serikali imetumia zaidi ya Sh. bilioni 3.4, kujenga kituo hicho na kununua vifaa vya ufundishaji  ili kuwainua vijana wa kike ambao hawawezi kufanya kazi ngumu za uchimbaji madini.
 
“Nasema hivi  kwa sababu  ukimfundisha  aliyesoma zaidi ya hapo, atakuwa na diploma  na digrii zake, ambazo hatataka kufanya kazi ya kushika kwa mkono, lakini hawa wa darasa la saba watafanya tu, hivyo vema wakafundishwa hawa kazi hii,”alisema.
 
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,  Mrinia Mchovu, alisema kituo hicho kimeanzishwa ili kuongeza thamani ya madini nchini.
 
Alisema serikali itaendelea kukiboresha kituo hicho kwa kutoa kozi za utengenezaji mapambo ya madini na uchongaji wa vinyango vya mawe ya madini ili kuongeza kipato kwa mfanyabiashara na serikali.
 
 Kamishna  wa  Madini, Mhandisi Paul Masanja, alisema serikali imejenga kituo hicho kwa zaidi ya  Sh.bilioni  1.2 na kununua vifaa vya kufundishia Sh. bilioni 2.1.
 
CHANZO: NIPASHE

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top