TANGAZO
Akinamama
wawili walioolewa na mme mmoja Bw, Shingu Mashigina, wamekufa kwa
wakati mmoja,ambapo mmoja akimpiga mwenzake na Mchi Kichwani na kufa
papo hapo,na kisha yeye aliyefanya mauaji, kujinyonga kwa kutumia kanga
katika nyumba hiyo hiyo huko katika kijiji cha Tura wilayani Uyui Mkoani
Tabora.
Akithibitisha
mauaji hayo mara baada ya kutoka katika mazishi ya akinamama hao
mtendaji wa kijiji Bw. Masabo Williamu amewataja marehemu kwa majina ya
Mindi Salmu (18) mke mdogo aliyeuawa, na Mwenda Kulwa (30),aliyejinyonga
baada ya kufanya mauaji ambapo chanzo cha mauaji hakikufahamika mara
moja.
Kamanda
wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda amethibitisha
kutokea kwa mauaji hayo ya kutisha huku akiitaka jamii kulaani kitendo
hicho cha kinyama kilichofanywa na mama huyo kisha kujinyonga.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment