} });
 

TANGAZO



MBUNGE wa jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Eugen Mwaiposa (CCM) amefariki dunia nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana akiwa usingizini.
Taarifa ya kifo hicho ilitolewa jana mchana katika kikao cha Bunge mjini hapa na Naibu Spika, Job Ndugai.
“Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepata msiba…” alisema Ndugai wakati alipokuwa analitangazia Bunge kifo hicho.
Alisema kwamba mbunge huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na kwamba maiti yupo Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi. Aidha, alisema kwamba mbunge huyo ataagwa leo nyumbani kwake Chadulu.
Nyumba yake imetazamana na Hoteli ya Shabib, barabara ya kwenda Dar es Salaam. Taarifa ya kifo chake ilitolewa wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Kikao cha Kumi na Tisa.
Wakati majadiliano yanaendelea, habari za kifo zilianza kusambaa na kabla mchangiaji Deo Sanga hajazungumza, Mwenyekiti wa Bunge Lediana Mng’ongo alimtafadhalisha mbunge kuketi kwanza hadi Naibu Spika atakapoketi.
Ndugai alisimama na kutoa taarifa ya kifo hicho na kuliahirisha Bunge hadi kesho asubuhi. Baadhi ya wabunge waliokuwa naye jana walisema kwamba hawakuweza kudhani kwamba mwenzao atafariki kwani alikuwa na siha njema.
Mbunge wa Kilosa na Waziri wa zamani wa Fedha, Mustafa Mkulo alisema kwamba juzi asubuhi walikuwa wanakunywa chai pamoja katika kantini ya Bunge na kutaniana na wala hakufikiria kwamba leo (jana) atapata taarifa ya kifo.
Mbunge huyo wa Ukonga ambaye mwaka huu pia alipania kutafuta ridhaa ya wana Ukonga kurejea tena bungeni, anasifika kwa uchapakazi wake.
Mbunge huyo akihojiwa hivi karibuni alisema kwamba anasubiri kwa hamu kubwa uchaguzi, kwani kwa kipindi chake cha ubunge ameweza kutimiza asilimia 80 ya ahadi zote alizotoa kwa wananchi wake.
Eugen alizaliwa Novemba 23, 1960 huko Hai mkoani Kilimanjaro na ni mama wa watoto wawili wa kike.
Katika kipindi chake tangu alipoingia bungeni mwaka 2010, amefanikisha pamoja na wananchi ujenzi na ukarabati wa vituo vya Polisi, uchimbwaji wa visima 21 jimboni kwake , ujenzi wa ofisi 11 za walimu wa shule mbalimbali za msingi na sekondari za serikali na ugawaji wa madawati katika shule za jimbo lake.
Eugen, mke wa Ally Ibrahim Mwaiposa, alipata elimu yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Uchumi cha Karl Marx kilichopo Sofia, Bulgaria na Strathclyde, Uingereza.
Atakumbukwa kwa namna ambavyo anapenda michezo na maswali yake bungeni. Habari kutoka nyumbani kwake, Chadulu, zilisema kwamba ilibidi majirani wakiongozwa na mbunge Betty Machangu wavunje mlango ili kutambua kulikoni baada ya kumsubiri kuamka hadi saa 3 asubuhi bila mafanikio.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top