TANGAZO
Taarifa ya TFF kwa waandishi wa habari jana ilisema uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya JB Belmonte (PSPF) iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo ilisema, katika hafla hiyo TFF itawatunukia vyeti viongozi mbalimbali waliotoa mchango katika mpira wa miguu, wadhamini, wahamasishaji pamoja na wachezaji waliochezea Taifa Stars ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu Tanzania kujiunga na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Viongozi wa kitaifa watakaotunukiwa vyeti ni marais wastaafu na wa sasa akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete.
Wengine ni rais mstaafu Abeid Amani Karume, Amani Abeid Karume, Abdul Wakili, Abdu Jumbe, Dk Salmin Amour na Dk.Ali Mohamed Shein.
Aidha TFF itatoa vyeti kwa watangazaji na waandishi wa habari za michezo wa zamani, timu ya taifa iliyofuzu michuano ya mataifa Afrika iliyofanyika Lagos, Nigeria mwaka 1980 wakiongozwa na rais wa zamani wa TFF Leodegar Tenga.
Vyeti pia vitatolewa kwa wenyeviti na marais wa zamani wa TFF, makatibu wakuu, makocha wa timu za taifa, wachezaji na mawaziri wa michezo na wadhamini.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment