TANGAZO
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi chawachezaji 23 watakaoondoka leo jioni kuelekea
Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka kambi ya
wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mholanzi
huyo amesema watatumia kambi ya Ethiopia
kujiandaa na mchezo wa Misri, vijana wapo
katika hali nzuri na wameahidi kupambana
kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa
kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El
Arab jijini Alexandria, ikiwa ni mchezo wa
kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika
(AFCON) mwaka 2017.
Kikosi cha Stars kinaondoka saa 11 jioni kwa
Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa
kuwasili jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni
kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini Ethiopia
Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali,
walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto
Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji,
Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum
Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said
Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John
Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,
Mrisho Ngassa na Juma Liuzio.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na
Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.
Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF
Vedastus Lufano amesema timu inakwenda
kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana
katika mchezo dhidi ya Misri.
Kikosi kingine cha timu ya Taifa kitaondoka
nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwand
kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya
Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya
Kimbali.
Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi cha
wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya
mchezo huo wa kirafiki, akisaidiwa na kocha
Bakari Shime.
Wachezaji watakaondoka kwenda Rwanda ni
Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel
Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka,
Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Rashid
Mandawa, Atupele Green, Kelvin Friday, Hassan
Kessy, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu, Mudathi
Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemb
na Mohamed Hussein.
nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwand
kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya
Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya
Kimbali.
Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi cha
wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya
mchezo huo wa kirafiki, akisaidiwa na kocha
Bakari Shime.
Wachezaji watakaondoka kwenda Rwanda ni
Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel
Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka,
Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Rashid
Mandawa, Atupele Green, Kelvin Friday, Hassan
Kessy, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu, Mudathi
Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemb
na Mohamed Hussein.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment