} });
 

TANGAZO

Pius Msekwa.
Umoja wa Madereva Tanzania (UMT), umesitisha mgomo baada ya wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kupitia chama chao cha Taboa kuahidi kuwapa mikataba ya ajira ambayo awali haikuwapo na kuwafanya wafanye kazi bila mikataba.
 
Ahadi hiyo ilitolewa jana na wamiliki hao baada ya kikao kilichowakutanisha Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi kavu (Sumatra), Wamiliki wa Mabasi ya Daladala (Darcoboa), Jeshi la  Polisi, UMT na Wizara ya Kazi na Ajira.
 
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana baada ya kumaliza kikao hicho, Katibu Mkuu wa UMT, Rashid Saleh, alisema wamiliki wamekubali kutoa mikataba ingawa hawajazungumzia masuala ya posho na mishahara.
 
“Baada ya kuvutana katika kikao hiki, wamiliki wamekubali kutupa mikataba, lakini bado masuala ya posho na mishahara ya ndani na nje ambayo tunataka tukae na tujadili tena hadi ifikapo Julai Mosi mwaka huu tuwe tumeshakubaliana mambo hayo ambayo bado,” alisema Sarehe.
 
Alisema kutokana na kutokuwa na mikataba kwenye kazi, wamekuwa wakifanya kazi kwa kunyanyaswa na waajiri wao.
 
NIPASHE ilipomtafuta Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu, alisema yeye sio msemaji wa kikao hicho bali anayetakiwa kuzungumzia suala hilo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira.
 
Madai ya maderera hao ni pamoja mikataba, posho, mishahara, utaratibu wa nauli ya kwenda na kurudi majumbani baada ya kazi, likizo, matibabu, usafiri na bima.
CHANZO: NIPASHE

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top