} });
 

TANGAZO

UONGOZI wa Yanga jana umemtambulisha mchezaji mpya waliyemsajili, Malimi Busungu na kusema kuwa sasa wanahamia kwenye usajili wa kimataifa.
Busungu, ambaye msimu uliopita alifanya vizuri akiwa na Mgambo Shooting, alisajiliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Mgambo kumalizika mwishoni mwa msimu.
Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema walivutiwa na kiwango cha Busungu alichoonesha katika timu yake ya Mgambo na hivyo kuamini kuwa atawasaidia katika mechi za kimataifa.
“Sisi kama Yanga tunapenda kusema kuwa tulivutiwa na kiwango cha Busungu, kazi tuliyopewa tumeimaliza na tumempa jezi namba 16 ambayo aliichagua mwenyewe,” alisema.
Busungu alikabidhiwa jezi iliyokuwa ikivaliwa na Nizar Khalfan ambaye mkataba wake umekwisha Yanga. Mchezaji huyo inadaiwa tayari amepata ulaji katika timu ya Mwadui Fc na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Jerryson Tegete.
Usajili wa Busungu utafanya idadi ya waliosajiliwa msimu huu kufikia wanne baada ya Deus Kaseke, Benedicto Tinoko na Haji Mwinyi.
Muro alisema baada ya Busungu wanahamia kimataifa ambapo tayari wamefanya mazungumzo na wachezaji mbalimbali na kwamba hivi karibuni watawatambulisha.
Miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa kusajiliwa ni Donald Ngoma wa FC Platinum ya Zimbabwe.
Alisema usajili wa wachezaji wengi wa kimataifa utaendelea kutegemea na ombi lao la kusajili wachezaji wanane wa kimataifa kama litapitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Muro alisema mchezaji huyo ni wa kiwango cha dunia na kwamba huenda akasajiliwa kwa vile kiwango chake ni cha kutisha.
Kwa upande wa Busungu alisema anawashukuru viongozi wa Mgambo na wachezaji wake kwa kushirikiana vizuri kama ndugu msimu uliopita hivyo ataendelea kuwakumbuka.
Alisema anashukuru kwa kupata timu inayoshiriki mashindano ya kimataifa kwa vile ilikuwa moja ya malengo yake kucheza kimataifa.

“Nashukuru Yanga waliniona baada ya kufanya vizuri msimu uliopita, nimefurahi kwa sababu nitacheza katika timu inayoshiriki mashindano ya kimataifa, nimejipanga na niko tayari kwa mapambano,” alisema.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top