} });
 

TANGAZO
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetaka watanzania wanaotumia vifaa mbalimbali vya upimaji, kutoridhishwa na upya wake, bali wawasiliane nalo livihakiki usahihi wake.
Aidha, limewataka wafanyabiashara wa vifaa vya upimaji nchini, kuepusha wanunuzi na watumiaji wa vifaa hivyo kupata matokeo yasiyostahili, kwa kuwa wa kwanza kuvifikisha kwenye maabara ya upimaji ili vifanyiwe uhakiki.
Msemaji wa shirika hilo, Roida Andusamile alisema Dar es Salaam hivi karibuni kuwa watanznaia wengi hawaitumii maabara ya vipimo iliyoko katika shirika hilo kwa ajili ya kuhakiki vifaa vya vipimo wanavyo vitumia, jambo linaloonesha kuwa wanaridhika navyo, bila kuwa na uhakika navyo.
Kwa mujibu wake, kifaa chochote cha upimaji hata kama ni kipya kinaweza kuwa na kasoro za kiufundi hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho, yatakayowezekana tu baada ya kukipima kujua ukubwa wa kasoro.
“Hivi karibuni shirika litaanza msako wa vifaa visivyofaa kutumika kufanya vipimo katika hospitali zetu, kuhakikisha kuwa wagonjwa hawapewi majibu ya vipomo yasiyo sahihi. Lakini, kabla ya kufanya hivyo, tunawashauri wenye vifaa hivyo wavilete tuvihakiki,” alisema.
Aidha, aliongeza kuwa, mmiliki au mtumiaji wa kifaa hapaswi kujidanganya kuwa anaweza kutambua makosa ya kifaa chake, kwa kuwa yanahitaji utaalamu na vifaa maalumu kuyagundua.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top