} });
 

TANGAZO

Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amewasimamisha kazi askari watatu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kwa kashfa ya wizi wa  mafuta ya ndege aina ya JET – A 1 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
 
Waliosimamishwa ni Khalfan Kisana na Musa Mandauli, ambao walikamatwa  Oktoba 7, mwaka jana, saa mbili asubuhi wakitumia gari aina ya Landrover la Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto,  lenye namba za usajili STJ 2948. Mwingine ni Abias Mwanza, aliyakamatwa kuiba mzigo wa abiria.
 
Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na madumu 10 yenye ujazo wa lita 20 za mafuta katika eneo la kiwanja hicho, karibu na geti la jeshi namba 603.
 
Akizungumza jana, baada ya ziara aliyoifanya kwa lengo la kukagua vikosi mbalimbali sambamba na kuhakikisha usalama, Masauni  alisema watuhumiwa hao wanatakiwa kusimamishwa mara moja na kupisha uchunguzi. Alisema iwapo watabainika kuhusika na matukio hayo,   hatua za haraka za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
Alisema Mwanza amesimamishwa kwa tuhuma za kuiba mzigo wa abiria Agosti 26, 2014 majira ya saa nane usiku.
 
Masauni alisema kuwa askari huyo alinaswa na kamera za usalama zilizoko uwanjani hapo. Alionekana akishirikiana na mfanyakazi wa kampuni ya Swissport, Lucas Maganda.
 
Alisema watuhumiwa hao walinaswa na kamera hiyo eneo la Cargo.  Mfanyakazi wa kampuni hiyo alionekana akimpigia simu askari huyo aliyekuwa nje, mara askari huyo akaja akiwa na pikipiki na kuchukua mzigo wa abiria ambaye hakujulikana.
 
Akizungumzia tukio lingine la wizi uwanjani hapo, Naibu huyo alisema Januari 13, mwaka huu,  yalionekana madumu 10 ya plastiki katika gari lenye namba za usajili T 225 AWN  yakiwa tupu huku dereva  aliyekuwa akiendesha gari hilo kutokuonekana. 
 
Lakini pia katika upande wa geti namba 8 lililoko uwanjani hapo, yalikutwa madumu ya plastiki takriban 30 ambayo nayo yalikuwa tupu katika gari lenye namba za usajili T 786 AWZ, Januari 18, mwaka huu.
 
Aidha Masauni alitoa agizo kwa jeshi hilo kutoa taarifa ndani ya siku 14 kuhussiana na wahusika waliosimamishwa sambamba na magari yaliyokamatwa yakiwa na madumu ya mafuta. Pia alitaka watoe taarifa ya mikakati endelevu katika viwanja vyote nchini, itakayosaidia kuondoa taswira mbaya dhidi ya jeshi hilo.
SOURCE: NIPASHE

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top