TANGAZO
Serikali imetoa zaidi ya Sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya ruzuku kwa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi mkuu 2015, vyenye sifa ya kupata fedha hizo.
Kadhalika, serikali imetoa zaidi ya Sh. bilioni 5.1 kwa ajili ya Mfuko wa Jimbo, za kuchochea maendeleo ya eneo husika.
Kwa mujibu wa taarifa ya mapato na matumizi ya serikali iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, serikali imekusanya Sh. 1,404,268,000,000 kutokana na kodi, mapato yasiyo ya kodi na vyanzo vya halmashauri.
Alisema pia serikali inatarajia kupata mikopo na misaada kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutoka kwa washirika wa maendeleo Sh. bilioni 71.2.
DK.Mpango alibainisha kuwa matumizi ya fedha hizo ni zaidi ya Sh. bilioni 484.1 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa ikijumuisha zaidi ya Sh.bilioni 9.5 za malimbikizo ya watumishi, hasa walimu katika halmashauri 154.
Pia alisema serikali italipa zaidi ya Sh. bilioni 97.9 za watumishi wa taasisi na wakala za serikali, ikijumuisha malimbikizo ya Sh.milioni 518.8 za taasisi na wakala 24 na sehemu kubwa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Waziri huyo alibainisha matumizi mengine kuwa ni miradi ya umeme ya thamani ya zaidi ya Sh.bilioni 73.2, kati yake ikiwa zaidi ya Sh. bilioni 24 za umeme vijijini, mradi wa umeme Kinyerezi 1 zaidi ya Sh. bilioni 43.8 na mradi wa kufua umeme Makambako hadi Songea Sh. bilioni 5.5.
Matumizi mengine, kqwa mujibu wa Dk. Mpango, ni malimbikizo ya madeni ya makandarasi wa barabara zaidi ya Sh. bilioni 166.9 na miradi ya maji zaidi ya Sh. bilioni 10.9.
Pia alisema zaidi ya Sh. bilioni 43.5 ni posho ya chakula kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na usalama; posho ya madaktari wanafunzi zaidi ya Sh. bilioni 1.7 na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa muhula wa tatu zaidi ya Sh. bilioni 57.
Dk. Mipango alisema zaidi ya Sh. bilioni 18.8 zimeelekezwa kwenye utekelezaji wa elimu bure; Sh. bilioni 2.6 za Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
Aliongeza kuwa zaidi ya Sh. bilioni 43.5 zimeelekezwa halmashauri kwa mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo na uendeshaji wa ofisi.
Waziri huyo alisema zaidi ya Sh.bilioni 3.6 zimeelekezwa katika kulipa madeni ya watumishi wasio walimu katika halmashauri; zaodi ya Sh.bilioni 2.6 za mfuko wa reli.
Alibainisha kuwa zaidi ya Sh. bilioni 3 zimeelekezwa kulipa fidia wananchi kupisha mradi wa Kurasini Logic Center na zaidi ya Sh. Bilioni 2.1 wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
SOURCE: NIPASHE
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment