} });
 

TANGAZO


Hatimaye kilio cha wakulima wa Tumbaku cha kukwama kuuza tumbaku yao kimemalizika baada ya msimu wa kuuza zao hilo kufunguliwa jumatano Juni 03 Mwaka huu katika mkoa wa kitumbaku wa Kahama
Hali hiyo imeelezwa leo mjini Kahama na mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika KACU Peter Emmanuel kuwa msimu huo utafunguliwa siku hiyo ya Jumatano hali ambayo itaondoa malalamiko ya wakulima hao kulalamikia kuchelewa kwa msimu huo
Emmanuel amefafanua kuwa utaratibu wa uuzaji wa Tumbaku hiyo utakwenda kwa dola na sio shilingi kama ilivyolipotiwa hivi karibuni na vyombo vya habari kuwa tumbaku itauzwa kwa shilingi wakati pembejeo italipwa kwa dola
Mwenyekiti huyo amesema utaratibu wa kwenye mkataba ni ule wa kuuzwa zao hilo kwa dola sambamba na pembejeo hiyo kulipwa kwa dola hali ambayo itawanufaisha wakulima wa zao hilo kutokana na kupanda kwa fedha hiyo ya kigeni
Kabla ya hapo meneja wa bodi ya tumbaku Tanzania wilayani Kahama Albert Challe amesema tatizo la ucheleweshwaji wa ufunguzi wa msimu huo ulisababishwa na serikali kuchelewesha kuleta fedha za kuendeshea zoezi hilo
Katika msimu wa mwaka huu jumla ya kilo milioni 8 zinatarajiwa kuuzwa kwenye makampuni mbalimbali ya ununuzi wa zao hilo hali ambayo inaweza kubadili kiuchumi, maisha ya wakulima hao.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top