} });
 

TANGAZO


RAIS wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Leodegar Tenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Soka la Wanawake ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Tenga pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Kwa mujibu wa taarifa kwenye tovuti ya CAF, uteuzi huo umetokana na kikao cha Kamati ya Utendaji cha CAF kilichokutana Zurich, Uswisi Mei 26, 2015 ambacho kilikuwa na kazi ya kufanya uteuzi wa viongozi wa kamati mbalimbali za shirikisho hilo.
Mbali na kuongoza Kamati ya Soka la Wanawake pia atakuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ambayo Rais wake ni Suketi Patel toka Shelisheli.
Aidha Rais huyo wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati nyingine za maandalizi ya mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) na nyingine ya ushauri kwa vyama ambavyo ni mwanachama wa CAF.
Naye Rais wa TFF Jamal Malinzi ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20, kamati ambayo itakuwa inaongozwa na Amaduo Diakite wa Mali.
Pia CAF imemteua Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, ambayo itakuwa inaongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Zambia, Kalusha Bwalya.
Aidha Watanzania wengine walioteuliwa kuwa wajumbe katika kamati mbalimbali ni Lina Kessy (Kamati ya Soka la Wanawake), Crescentius Magori (Kamati ya Soka la ufukweni na viwanja vya ndani) DK. Paul Marealle, (Kamati ya Tiba) na Richard Senamtwa ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye Bodi ya Rufaa.

soma habar kilasiku kazi ya mikono yangu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 859 030 #ZAMU YAKO 2016

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top